Psalms 78:60-64


60 aAkaiacha hema ya Shilo,
hema aliyokuwa ameiweka katikati ya wanadamu.

61 bAkalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani,
utukufu wake mikononi mwa adui.

62 cAliachia watu wake wauawe kwa upanga,
akaukasirikia sana urithi wake.

63 dMoto uliwaangamiza vijana wao,
na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,

64 emakuhani wao waliuawa kwa upanga,
wala wajane wao hawakuweza kulia.

Copyright information for SwhKC